Polisi wafyatua risasi kuwatawanya waandamanaji Kisumu

Polisi wamefyatua risasi halisi mjini Kisumu wakiendelea kukabiliana na wafuasi wa Bw Odinga ambao wamefunga baadhi ya barabara, mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza aliye katika mji huo wa magharibi mwa Kenya anasema.

Watu wawili wamejeruhiwa - wote wawili wakiwa na majeraha ya risasi kwenye mapaja.

Waliojeruhiwa ni mvulana wa miaka 15 na mwanamume wa miaka 21.

Wawili hao wanapokea matibabu hospitalini.

Comments